
Friday, November 13, 2009
Mikumi Kukavu!
Nilidhani nitaona wanyama wengi wakati basi niliyopanda kwenda Kyela inapita katika mbuga ya wanyama, Mikumi. (Mikumi National Park) mkoani Morogoro. Naona moto uliteketekeza mbuga hiyo. Ilikuwa kavu, mito imekauka kabisa, yaaani ilisikitisha kabisa kupita pale Mikumi. Ila niliweza kuona twiga watatu, punda milia mmoja na swala kama ishirini.

