Wadau, nimerudi Boston. Siku ya jumamosi nilikuwa sijisikii vizuri nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu pale Tangi Bovu. Ilikuwa nikitembea kidogo nachoka. Mama yangu kasema niende Massana Hospital kupima damu. Nilienda jumapili asubuhi kupima. Kweli nilikutwa na Malaria! Duh! Nikapewa tiba. na kuondoka mchana huo huo. Yaani nadhani niliambukiwa siku ya kwanza nilivyokuwa Dar.
Chandarua ya dawa, dawa ya kuzuia mbu ya kupaka, RUNGU, Anti-malarials (malarone) hazikuyfanya kazi!
Hata hivyo nategemea kurudi Tanzania mwakani na kukaa muda mrefu zaidi!