
Umewahi kuugua malaria Marekani? Usiombe maana ugonjwa ambao unatibika Bongo, inaweza kukuua hapa. Bora uje na dawa kutoka Bongo kabisa.
Hapa USA hawaelewi kabisa malaria ni ugonjwa wa aina gani. Nawambia huwezi kuipata kupitia kwenye hewa. Nikawaambia kuwa Afrika, m ugonjwa wa malaria ni common vile ugonjwa wa mafua hapa. Watu wengi tu wanapata. Nawaambia inaambukizwa na mbu, tena anopheles mosquito. Hapa Marekani hamna. Kuna siku niliwaambia watu weusi na wazungu wa hapa kuwa niliuugua malaria sana nikiwa Tanzania, wakanitazama kwa mshangao na woga. Utadhani walikuwa wanamtazama Frankenstein yule monster wa kwenye masinema!
Nafahamu wazungu kama wanne ambao wamekufa nao hapa. Kisa madaktari hawakujua wanaumwa nini. Wali safiri nchi zenye malaria na kuugua baada ya kurudi. Pia mara nyingi madatari wa Marekani hawa uzoefu na huo ugonjwa ambao Tanzania ni kama kuugua mafua hapa.
Kuna MBongo kanisimulia kuhusu alivyokuja tu kutoka Bongo miaka ya 80, New York. Anasema alianza kujisikia vibaya na akaenda clinic. Kamwambia daktari kuwa anadhani ana malaria, maana katoka Tanzania hivi karibuni. Heh! Kosa kubwa. Kajaza fomu kwenda CDC (Center for Disease Control). Anasema manesi walikuwa wanamwogopa. Wakawa wanauliza kama wanaweza kuambukizwa. Anasema daktari hakuwahi kutibu malaria na ilibidi angalie kwenye kitabu na kumwandikia prescription ya quinine! Damu ilipimwa na ilichukua siku tatu kupata majibu. Haikuisha hapo, anasema alivyofika nyumbani katembelewa na health officer wa serikali. Wakamwuliza maswali mia kidogo mpaka kaogopa kuwa atarudiishwa Tanzania.
Bahati nzuri haikuwa na malaria wakaacha kumsumbua.
Lakini hivi karibuni kuna jamaa alienda Tanzania, karudi na malaria. Akashindwa kwenda kazini , alichukua siku mbili off na kupiga simu kuwa amerudi kutoka safari lakini anaumwa. Alivyoenda kazini, bosi kamwuliza alikuwa anaumwa nini, jamaa kamwambia, alikuwa na malaria. Heh! Utadhani jamaa alimwambia anaumwa Ebola virus. Jamaa alifukuzwa kazi. Nikamwambia bora ungemwambia unflu au UKIMWI, kulikoni umwambie kuwa una malaria.
Na kuna dada fulani naye aliuugua, tena alipata attack ya kusikia baridi na kutetemeka akiwa kazini. Kazi aliyokuwa anafanya ni ya kuangalia wazee. Huyo alikuwa na bahati walimpa paid leave ya wiki tatu! Lakini aliniambia kuwa alijuta kwa nini aliwaambia maana watu walikuwa kama wanamwogopa.
Naona siku hizi mambo kidogo afadhali, maana kuna tropical disease experts wengi. Wengine walifanya practicals kwenye mahospitali za Afrika na hata Tanzania. Lakini ukimkosa mtaalamu wa kukutibu, Mungu akulinde.
Karibuni mtoe maoni yenu au story zenu za malaria Marekani.