

Leo kuna habari ya fujo zilizotokea huko Afrika Kusini. Wanasema kuwa wananchi wenye hasira wanaua wageni/wahamiaji kutoka nchi zingine amboa wako kwao. Mpaka sasa watu 22 wameuliwa. Kisa eti ni chanzo cha wao kukosa kazi! Wengi ya waliouliwa wanatoka nchi za kiafrika kama Zimbabwe, Mozambique na Malawi.
Wageni huko wanakimbilia vituo vya polisi na makanisani kuomba hifadhi kusudi wasiuliwe.Hivi Afrika Kusini imelaaniwa nini? Watu ni wepesi kusahau. Miaka mingapi Tanzania na nchi nyingi za dunia ziliwasaidia waAfrika Kusini mpaka walivyopata Uhuru wao. Mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyozuia timu ya Olympiki ya Tanzania kushiriki katika michezo kwa vile Wazungu kutoka Afrika Kusini walikuwa wanashiriki wakati weusi huko wananyanyaswa na Apartheid? Mnakumbuka Dakawa na Mzimbo huko Morogoro? Na tusisahau hao WaSouth Africa walioacha mbegu Bongo!
Hebu tukumbuke ni MSouth Africa aliyesababisha ajali iliyotoa roho mpendwa Waziri Mkuu wetu, Edward Moringe Sokoine! Na yule jamaa yuko wapi? Je, ni moja wa hao wanaotaka kuona waBongo huko wanauliwa!
Askofu Desmond Tutu amewaomba waache kuua watoto wa watu waliowasaidia kutoka kwenye mikono ya Apartheid. Ni aibu!
Kwa habari zaidi someni:
http://www.iol.co.za/index.php?set_id=1&click_id=15&art_id=vn20080520055831988C677548
http://voanews.com/english/2008-05-19-voa31.cfm
http://www.cnn.com/2008/WORLD/africa/05/19/southafrica.deaths/index.html?iref=mpstoryview
http://ap.google.com/article/ALeqM5gmIvAinmgwYn-UUN6RYP_l1wNu_QD90OR8P80
http://voanews.com/english/2008-05-19-voa31.cfm
http://www.cnn.com/2008/WORLD/africa/05/19/southafrica.deaths/index.html?iref=mpstoryview
http://ap.google.com/article/ALeqM5gmIvAinmgwYn-UUN6RYP_l1wNu_QD90OR8P80