





Watu wanangojea kwa hamu sinema ya Bongoland II.
Kwenye crew ya Bongoland II kulikuwa na mtaalamu wa mambo ya stunts (kupigana, kuanguka nk katika sinema) anaitwa Jason Hilton. Nilivyokuwa Bongo niliwaambia baadhi ya wasanii kuwa wawe makini kujifunza maana alikuwa anatoa somo bure. Hapa Marekani ukitaka masomo ya stunt unalipia hasa.
Kwa kweli kuna umuhimu wa mwalimu wa kufundisha stunts kwa wasanii Bongo. Nilishangaa sana nilipoambiwa kuwa eti katika sinema za Bongo, ukiona watu wanapigana au mtu kazabwa kibao basi wanafanya kweli hadi kuumizana! Hollywood mnaona watu wanapigana kumbe hakuna mtu aliyeguswa. Mfano kwenye ile sine ya Aftershock:Beyond the Civil War ambayo nimo, utadhani jamaa wanapigana kweli. Kumbe jamaa hakuguswa hata kidogo. Nakumbuka walivyoifilm na final product nikashangaa kweli utadhani jamaa kaua!
Website ya Jason Hilton ni: http://www.tumblemonster.com/pages/gallery.html
Hapa mnaweza kuona clip fupi ya mapingano kutoka sinema ya Bongoland II.
Note inachukua muda ku-load.
http://www.tumblemonster.com/video/TMPStuntSchoolReel.mov